Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Channel Catalog


Channel Description:

UBORA NI WETU - KARIBU NYUMBANI

older | 1 | .... | 99 | 100 | (Page 101)

  0 0

  Bilashaka moja kati ya stori inayoendelea kuwaacha watu wengi midomo wazi ni hii ya Mzeze mwenye umri wa miaka 80, Kofi Asilenu raia wa Ghana ambaye ana watoto 100 amedai bado anahitaji kuongeza watoto wawili katika familia yake.

  Asilenu ana wake 12 na anaishi na familia yake katika kijiji cha Amankrom kilicho umbali wa kilomita 45 kutoka mji mkuu wa nchii hiyo, Acca. 
  Familia yake ni thuluthi moja ya watu 600 katika kijiji anachoishi.

  Sababu ya yeye kutaka kuendelea kuzaa ameeleza kuwa anahitaji familia kubwa kwa sababu hapo awali hakuwa na ndugu, “sina kaka wala shangazi, ndio sababu niliamua kuwa na watoto wengi ili nipate maziko mazuri nikifa,” alisema Asilenu.

  0 0


  A post shared by Beyoncé (@beyonce) on
  Dunia imekuwa ikisubiria kwa hamu kuona watoto wa mapacha wawili wa mastaa Beyonce (35) na Jay Z (47), ambapo leo Ijumaa Queen Bey amevunja ukimia kupitia account yake ya Instagram na kuweka picha yake akiwa amebeba mapacha wao.

  Kati ya mastaa walio like picha hiyo ni pamoja na Kim Kardashian, ambae familia yake kwa siku za usoni hawakuwa na mahusiano mazuri.

  0 0

  Moja kati ya stori kama wewe ni shabiki wa filamu za Kihindi, hii ya staa wa filamu kutoka katika kiwanda cha filamu Bollywood India, Priyanka Chopra baada ya picha hizi na kipande cha video kuvuja akionekana Location "New York City’s Central Park" nchini Marekani na staa wa Hollywood.
  Wiki hii Staa Priyanka Chopra amekuwa location akishuti filamu yake mpya kutoka Hollywood inayoitwa "Isn’t It Romantic"? aliyomshirikisha staa wa hollywood Adam DeVine, picha unazoziona hapo niwakati wakiwa katika uigizaji.

  Sasa chungulia hapo video iliyosemekana kuvuja wakati wanaigiza video hiyo>>>


  0 0

  Hii inakuwa mara ya kwanza kwa mwanadada Jacqueline Fernandez na mkali Sidharth Malhotra kuigiza pamoja katika movie hii inayokwenda kwa jina la Gentlemen inayotarajiwa kuachiwa rasmi mwezi August 25th, 2017.

  Sasa kama wewe ni shabiki wa movie za Kihindi, huu ndio mtonyo ambao unapaswa kuufahamu wakwetu, ambapo hiyo hapo juu ndio poster official ya Gentlemen.

  0 0

  Magazeti, Redio, Tv na mitandao ya kijamii vimeonekana kumzungumzia muigizaji mkongwe na  anayefanya vizuri kwenye soko la filamu India, Sanjay Balraj Dutt, aliyekuja nchini kwa ajili ya mapumziko anatarajiwa kudumu kwa siku 21 ambapo atatembelea mbuga za wanyama na vivutio mbali mbali vilivyopo nchini. 

  Ujio wa Sanjay Dutt umethibitishwa na mwenyeji wake ambaye ni Mbunge wa Manonga, Seif Gulamali ambaye amesema uwepo wa msanii huyo ni kipimo cha kuwa sekta ya utalii nchini inaendelea kupanuka.
  Muigizaji Sanjay Dutt (kushoto) akipeana mkono na Mbunge Gulamali
  "Uwepo wa Sanjay Dutt nchini ni fursa kubwa sana.Wahusika wa utalii hapa nchini wakiona fursa katika kuutangaza zaidi utalii wetu ni vyema pia wakamtumia kwani mtu huyu ni mkubwa sana kwenye sanaa ya filamu. 

  Lakini pia kuja kwake hapa nchini ni wazi tunazidi kukua kwenye sekta hii, na tutapata mapato kupitia kuwepo kwake kwani atakuwepo kwa takribani siku 21" alisema Mhe. Gulamali
  Hata hivyo mbunge huyo amewataka waigizaji wa filamu nchini kuchangamkia fursa ya kukutana na muigizaji huyo kwa ajili ya kupata madini yatakayowasaidia kukuza na kupanua soko la filamu.

  Sanjay Dutt amefika Arusha mapema jana akitokea Dar es salaam kwa ajili ya kuzuru mbuga za wanyama, Ngorongoro, Serengeti, mbuga ya Selou na vivutio vingine vilivyopo nchini.
  Chanzo: Eatv

  0 0

  Asili Yetu Tanzania Blog kupitia kurasa zake za mitandao ya habari online, inapenda kukutaarifu ewe mkulima, mjasilia mali na mtu yeyote unayehita shughuli yako ifahamike na mamilioni ya watukupitia mitandao yetu online (Asili Promo), unakaribishwa kuchangamkia ofa hii maalu.

  Kutokana kuwa tunauzalendo na nchi yetu Tanzania, basi ASILI YETU TANZANIA BLOG kupitia kitengo chake cha promotion (Asili Promo) imetoa punguzo maalum la kutangaza shughuli yako katika msimu huu wa sikukuu ya wakulima NANE NANE.

  Ziko ofa nyingine nyingi utakazozipata (mteja wetu) endapo utatangaza nasi, aidha kwa kupost habari yako katika mtandao wetu au kuweka tangazo asilia, litakaloonekanakwa mamilioni wa folower wetu.

  Kwa mawasiliano zaidi tumia hizo namba hapo juu kwenye banner.

  0 0

  Mfuko moja uliotumika na mwananga Neil Amstrong kukusanya violezi vya mwezi, umeuzwa kwa dola milioni 1.8 mjini New York.
   
  Mfuko huo katika chombo cha angani cha Apolo 11 mwaka 1969 ulinunuliwa katika eneo la Sotheyby na mtu asiyejulikana.
   
  Mfuko huo bado una vumbi na mawe madogo madogo kutoka mwezini.
   
  Mnada huo unajiri baada ya mapambano mahakamani kuhusu umiliki wa kifaa hicho cha kipekee kutoka Apollo 11 ambao ulikuwa katika mikono ya mtu binafsi.
   
  Baada ya chombo hicho cha angani kurudi duniani, vifaa vyote vilipelekwa katika jumba la makumbusho la Smithsonian.
   
  Hatahivyo mfuko huo uliachwa katika boksi katika kituo cha vyombo vya angani cha Johnson kutokana na makosa ya kihesabu.
   
  Baadaye haukutambulika wakati wa mnada wa serikali, ukiuzwa kwa dola 995 pekee kwa wakili mmoja wa Illinois 2015.
   
  Hatahivyo mamlaka inayosimamia vyombo vya angani Nasa ilijarabu kuuchukua mfuko huo, lakini mapema mwaka huu, jaji mmoja aliamuru kwamba, ulimilikiwa na mnunuzi huyo kimakosa ambaye baadaye ailiupeleka katika mnada huo wa Sutheby.
  Chanzo: BBC


  0 0

  Tanzania imetajwa kuwa kivutio kizuri cha safari za watalii barani Afrika kulingana na mtandao wa SafaricBookings.com ambao ndio mtandao mkubwa wa ukuzaji wa safari za Afrika.

  Mtandao huo ulifanya tathmini ya zaidi ya wataalam 2500 na wale walioshiriki katika safari hizo kabla ya kutangaza kuwa Tanzania ndio eneo bora la safari mwaka 2017.

  Tathmini hizo ziliandikwa na watalii walioenda safari pamoja na wataalam bingwa wa Afrika.

  Mtandao huo unasema kuwa, uchanganuzi huo pia ulibaini kwamba Tanzania ilipata umaarufu wake kutokana na idadi ya wanyama mbali mbali.
  Watu maarufu katika miezi ya hivi karibuni wamekuwa wakizuru Tanzania, kwa kwakutembelea maeneo tofauti ya vivutio vya utalii nchini Tanzania.

  Watu hao ni mwanamuziki maarufu Usher Raymond, aliyekuwa mchezaji wa klabu ya Manchester United na Real MadridDavid Beckham, aliyekuwa mchezaji wa Liverpool Mamadou Sakho, mchezaji wa EvertonMorgan Schneiderlin na nyota wa filamu kutoka Marekani Will Smith na Harrison Ford.

  Walitembelea mbuga za Serengeti na mlima kilimanjaro.
  Mtandao huo uliitaja Zambia kuwa taifa lenye kivutio kizuri cha misitu huku wataalam wote wakikubaliana kwamba mazingira ya
  misitu nchini humo mi mazuri zaidi.

  Vilevile Zambia pia ilitajwa kuwa taifa lenye maisha bora ya ndege.
  Namibia na Kenya zilitajwa kuwa bora katika mandhari mazuri pamoja na ndege waliopo mtawalia.

  Chanzo:BBC

  0 0

  Tiketi za kushuhudia mpambano wa masumbwi kati ya Floyd Mayweather dhidi ya Conor McGregor zinauzwa kwa dola 150,000.
  Mpambano huo unatajwa kuwa wa gharama zaidi kuwahi kutokea na tiketi kwa sasa zinauzwa kama njugu.

  Unatarajiwa kupigwa Agosti 26 katika uwanja wa T-Mobile mjini Las Vegas utakaoingiza watu elfu 20.

  Mayweather mwenye miaka 40 awali alistaafu mchezo wa masumbwi lakini amerejea tena kupambana na McGregor.

  0 0
 • 07/28/17--00:51: Video: Harmonize - 'Sina'
 • Msanii kutoka Wasafi Classic Baby maarufu kama Harmonize baada ya kuwa na collable kibao kupitia ngoma zake na nyingine alizoshirikishwa na wasanii wenzake, sasa ameachia video Mpya wa waimbo wake wa 'SINA'.

  Katika video hii mkongwe wa TAKEU STYLE Mr. Nice ameonekana.

  Utazame hapo chini>>>


  0 0

  Mwanzilishi wa Kampuni ya Amazon, Jeff Bezos amempita Bill Gates na kuwa tajiri namba moja duniani akimiliki utajiri wa dola za kimarekani 90.6 bilioni (Tsh 203 trilioni).

  Kupanda kwa hisa za Amazon kwa asilimia 1.5 Julai 27 kulimaanisha kuwa tajiri huyo amempita mwanzilishi mwenza wa Microsoft, kwa mujibu wa taarifa za jarida la Forbes la nchini Marekani.

  Forbes wameeleza kuwa Bezos ana utajiri wa $90.6 bilioni akimzidi Bill Gates aliyekuwa anashikilia nafasi hiyo akiwa na utajiri wa $90 billioni sawa na Tsh 201.5 trilioni.

  Bezos ananakadiriwa kumilikia hisa milioni 80 za Amazon akiwa ni mwenye hisa nyingi zaidi ya mwingine yeyote.

  Kwa miaka ya hivi karibuni amekuwa akijikita zaidi katika mradi wake wa Blue Origin unaohusika na urushaji wa rocket kwenda angani pamoja na Washington Post ambazo zote anazimiliki.

  Bezos ambaye ni Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu (CEO) wa Amazon alizaliwa mwaka 1964 Albuquerque Jimbo la New Mexico na alisoma Sayansi ya Kompyuta na Uhandisi wa Umeme katika Chuo Kikuu cha Princeton.

  Alipohitimu alikwenda kufanya kazi na Wall Street lakini mwaka 1994 aliacha kazi na kwenda kuanzisha Amazon ambapo kwa mara ya kwanza Amazon ilianzishiwa katika karakana ya kutengenezea magari. 

  Baada ya kampuni hiyo kuanza kufanikiwa na kujipanua katika nchi mbalimbali, mwaka 2000 alianzisha kampuni ya Blue Origin inayojishughulisha na masuala ya anga.

  Mwaka 2013 akiendelea kujipanua, aliinunua Kampuni ya Washington Post kwa dola milioni 250  na ilipofika Mei 2017 alitajwa kuwa na utajiri wa dola bilioni 84.8 , lakini leo Julai 27, 2017 amefikisha utajiri wa dola bilioni 90.6  na kushikilia usukani wa mtu tajiri zaidi duniani.

  Kwa mujibu wa Forbes, hawa ndio matajiri 10 wanaoongoza duniani;

  1. Jeff Bezos (53)- Amazon.com
  2. Bill Gates (61)- Microsoft
  3. Amancio Ortega (81)- Zara
  4. Warren Buffett (86)- Berkshire Hathaway
  5. Mack Zuckerberg (33)- Facebook
  6. Carlos Helu (77)- telecom
  7. Larry Ellison (72)- software
  8. Michael Bloomberg (75)- Bloomberg LP
  9. Bernard Arnault (68)- LVMH
  10. Charles Koch (81)- diversified

  0 0

  Mtandao wa kijamii wa WhatsApp umebainika kutumiwa na watu Bilioni moja kwa kila siku.

  Mnamo mwaka jana mtandao huo ulikuwa na watumiaji bilioni moja ila sasa idadi hiyo imekuwa ni ya wanaotembelea kila siku, inadaiwa kuwa katika watu kumi kati ya watu wanane hadi saba wanatumia mtandao huo. 

  Mitandao mingine inayoongoza kuwa na watumiaji wemngi kwa siku ni Facebook , Instagram na Messenger.

  Utafiti uliofanyika mwaka 2014 na Chuo Kikuu cha Pittsburgh cha Pennsylvania nchini Marekani, ulibaini  kuwa alisimia 71 ya wanotumia mitando ya kijamii  ni vijana na hutumia kila baada ya dakika 10.

  0 0

  Rais Mstaafu Jakaya Kikwete amezidi kuonyesha mfano katika kilimo baada ya kuonekana akiwa katika mashamba yake ya Mizabibu Dodoma
  Kupitia mtandao wa twitter Mh. Kikweteameandika,Nikiwa Dodoma nimepata wasaa wa kutembelea na kukagua shamba langu la mizabibu. Mwaka huu mavuno yatakuwa mazuri Insha Allah.
  June 4mwaka huu  pia alifanya hivyo kwa kuandika,Kuna maisha baada ya Urais hususani wasaa wa kufanya yale uliyokosa muda wa kuyafanya kama kutumia muda na familia,kuangalia mifugo na shamba”. 

   Kisha kuweka picha akiwa katika shamba lake la mahindi kijijini Msoga.

older | 1 | .... | 99 | 100 | (Page 101)