Quantcast
Channel: Www.maxwellyblogspot.com
Viewing all 3608 articles
Browse latest View live

Inasemekana kuendesha bodaboda muda mrefu ni hatari kwa afya ya uzazi

$
0
0
Vijana wengi Afrika Mashariki wamekuwa wakitumia baiskeli kufanya biashara ya uchukuzi wa abiria, maarufu kama boda boda.
Ni kazi inayohitaji mhudumu atumie nguvu nyingi za mwili wake.

Sasa, watafiti nchini Kenya wanasema kunaweza kuwa na changamoto nyingine - kwamba wahudumu wa bodaboda wanakabiliwa na hatari ya kupoteza uwezo wao wa uzazi.

Baada ya kufanya utafiti, waligundua kwamba waendeshaji boda boda walikuwa katika hatari ya kutoweza kutanua mishipa ya damu kwenye uume wakati wa kushiriki tendo la ngono.

Mmoja wa watafiti hao Isaac Wamalwa ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Jomo Kenyatta aliambia BBC kwamba suluhu huenda likawa ni kutumiwa kwa kiti maalum ya waendesha baiskeli ambayo hakitadhuru uume wa waendeshaji.

Bw Wamalwa ambaye ni mtaalamu wa masuala ya afya ya uzazi alifanya utafiti miongoni mwa vijana eneo la Bungoma, magharibi mwa Kenya.

Walichunguza wahudumu 115 wa boda boda wa umri wa chini ya miaka 40 eneo hilo, wakishirikiana na wataalamu wa afya ya uzazi kutoka Hospitali ya Taifa ya Kenyatta na Chuo Kikuu cha Nairobi.
"Tuliwachunguza vijana waendeshaji wa bodaboda Bungoma na matokeo yalikuwa ya kushangaza. 

Kwa jumla, tuligundua kwamba zaidi ya theluthi moja ya waendeshaji bodaboda, asilimia 35.9, ya washiriki walikuwa na matatizo ya kuweza kusimika," aliambia gazeti la Standard la Kenya.

Anasema tatizo lilitokana na kuendesha baiskeli hizo kwa muda mrefu.

Bw Wamalwa anasema wote walioendesha baiskeli kwa zaidi ya saa 60 kwa wiki, walikuwa na matatizo ya kiafya.
Anatahadharisha pia kwamba maelfu ya vijana wanaofanya mazoezi kwenye vituo vya mazoezi mijini, kwa Kiingereza gym, ambapo huendesha baiskeli zisizosonga, wanakabiliwa na hatari sawa na hiyo.

"Ujumbe wetu ni muhimu kwao pia, kwamba wanafaa kuwa wanapumzika kwa muda kutoka kwa kazi yao. Anasema wanapojikakamua kutafuta posho, wanafaa pia kujali uwezo wao kitandani."

Wataalamu wengine sita kutoka Chuo Kikuu cha Moi walifanya utafiti mjini Eldoret, magharibi mwa Kenya, na kupata matokeo
yanayokaribiana na ya Bw Wamalwa.

Waliwachunguza wahudumu wa dbodaboda 131 wa umri wa kati ya miaka 18 na 65, umri wa kadiri ukiwa miaka 40.
Waligundua kwamba asilimia 76 kati yao walikuwa na matatizo kitandani.

Watafiti hao pia walidokeza kwamba tatizo hilo huenda linatokana na kuendesha baiskeli kwa muda mrefu.
Stori na BBC

Mbwa wafurika katika vituo vya kupiga kura katika uchaguzi 2017 Uingereza.

$
0
0
Wapiga kura walipokuwa wanafika vituoni kupiga kura Uingereza, mbwa wa kila aina hawakuachwa nyuma.

Na punde si punde, watu walianza kugundua kwamba wanyama hao walikuwa wengi sana ajabu, na kitambulisha mada cha #DogsAtPollingstations (Mbwa vituo vya kupigia kura) kikaanza kuvuma mitandaoni.

Kando na mbwa, kunao watoto, paka na hata nungunugu walionekana na kuvutia watu vituoni.
Wengi walipakia picha za mbwa wao mtandaoni Alhamisi asubuhi na katika kipindi cha saa mbili za kwanza baada ya vituo kufunguliwa, ujumbe 8000 kuhusu mbwa ulikuwa umepakiwa mtandaoni.

Mtindo kama huo ulionekana katika uchaguzi wa mitaa mwezi uliopita, kura ya maoni kuhusu kujiondoa kwa Uingereza kutoka Umoja wa Ulaya na wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka jana.
Mwaka huu, Twitter hata walitoa kibonzo cha mbwa akiwa amevalishwa bendera ya Uingereza.

Twitter walishirikiana na wakfu wa The Dogs Trust kutetea kuwepo kwa mazingira bora ya mbwa kwenye vituo vya kupigia kura.
Stori na bbc

Orodha ya vyuo vikuu bora duniani kote kwa mwaka 2017.

$
0
0
Orodha mpya ya kila mwaka ya vyuo vikuu bora zaidi duniani imetangazwa, ambapo chuo kikuu cha Massachusetts Institute of Technology (MIT) cha Marekani bado kinaongoza.

Vyuo vikuu vya Stanford na Harvard - pia kutoka Marekani - kadhalika vimeendelea kushikilia nafasi ya pili na ya tatu mtawalia.

Orodha hiyo ilishirikisha vyuo vikuu karibu 1,000.

Vyuo vikuu hupimwa kwa mambo kama vile majarida na vitabu vya kisomi vilivyochapishwa, makala zilizonukuliwa, maoni ya wasomi pamoja na waajiri na pia ushiriki wa vyuo vikuu hivyo katika ngazi ya kimataifa.
Chuo kikuu cha Nairobi kimeorodheshwa kuwa kati ya nambari 801 na nambari 1000, kutoka kuanzia nambari 701 hadi 1000mwaka jana, sawa na Chuo Kikuu cha Makerere.

Vyuo vikuu 10 bora zaidi duniani kwa mujibu wa QS World University Rankings
  1. Massachusetts Institute of Technology (MIT)
  2. Stanford
  3. Harvard
  4. California Institute of Technology (Caltech)
  5. Cambridge
  6. Oxford
  7. University College London
  8. Imperial College London
  9. Chicago
  10. ETH Zurich

Msanii Rihanna atoa msaada wa milioni za dola katika elimu nchini Malawi.

$
0
0
Msanii wa muziki nchini Marekani Rihanna  ametoa msaada  wa kiasi cha Us dola milioni 20 nchi  Malawi kwa ajili ya kusaidia miundombinu  katika sekta ya Elimu.

Rihanna na kwa kushirikiana na GPforEducation, mwezi wa kwanza mwaka huu alitembelea nchi hiyo kwa lengo la kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu kupata elimu ili waweze kutimiza ndoto zao.

“My time in Malawi was so inspiring! Working with my @ClaraLionelFdn to improve the lives of students globally, alongside @GPforEducation… ”

Msanii huyo ameendelea kutumia muda wake pamoja na mali zake ili kuinua sekta ya elimu barani Afrika.

Tatizo la ukosefu wa miundominu haipo Tanzanzia pekee bali hata nchi zingine kwenye bara la Afrika.
Picha na video za msanii huyo zimeanza kusambaa kwa kasi siku ya jana zikumuonesha yupo Malawi.

Moto wateketeza nyumba takribani 150 Africa ya Kusini

$
0
0
Watu takriban 10,000 wamelazimika kukimbia makwao kutoka mji mmoja pwani ya Afrika Kusini ambao umeharibiwa pakubwa na moto.

Wanajeshi wanashiriki katika juhudi za kukabiliana na mtaa huo kukabili moto huo ambao unawaka katika maeneo 25 katika mji wa Knysna.

Watu wanane wamefariki kutokana na upepo mkubwa na moto ambao umekumba mji huo na maeneo mengine katika kanda ya Cape Magharibi.

Upepo huo mkubwa umesaidia kueneza moto huo.

Nyumba zaidi ya 150 zimeteketezwa eneo hilo kwa mujibu wa shirika la wazimamoto.

Mji huo una takriban wakazi 77,000.


Unapatikana kilomita 500 mashariki mwa mji wa Cape Town.

Jeshi la Taifa la Afrika Kusini litasaidia kuangusha mabomu ya maji yanayotumiwa kuzima moto kusaidia kukabili moto huo, msemaji wa jeshi Simphiwe Dlamini amesema.

Wanajeshi karibu 150 watatumwa eneo hilo kuzuia wahalifu kupora mali katika maeneo ambayo wenyewe wamekimbia.

Mwezi Mei, mkoa wa Cape Magharibi ulitangaza janga ya ukame baada ya mabwawa mawili makubwa kukauka kabisa.

Matokeo ya kidato cha tano na Vyuo vya Ufundi kwa mwaka 2017.

$
0
0
Simbachawene ametoa kauli hiyo jana mjini Dodoma wakati akizungumza na waandishi ws habari na kusema kuwa ufaulu kwa mwaka huu umeongezeka kwa asilimia 3.75 ukilinganisha na matokeo ya mwaka 2015.

Waziri amedai kati ya wanafunzi 96,018 waliofaulu kwa daraja la kwanza hadi la tatu ni wanafunzi 93,019 tu ndiyo waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi.

Waziri Simbachawene amesema kuwa jumla ya watahiniwa wote waliofanya mtihani wa kidato cha nne kwa shule kwa mwaka 2016 ni 349,524 huku waliofanya mtihani wa kujitegemea ni 47,751 ambapo watahiniwa waliofanya mtihani wa shule waliofaulu kwa daraja la kwanza hadi la tatu ni 96,018 sawa na asilimia 27.60 ya watahiniwa waliofanya mtihani Tanzania Bara.

Simbachawene alisema kutokana na mwongozo wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wa Mei 15, 2017 jumla ya wanafunzi 93,019 ndiyo wenye Sifa za kuchaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi kwa kuwa wamefaulu vigezo vyote vya msingi kama vilivyobainishwa na Wizara ya elimu sayansi na teknolojia ambapo kati ya hao 92,998 ni wa shule na wanafunzi 21 ni wale waliosoma taasisi ya elimu ya watu wazima.

Aidha amewataka wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano kuwasili kwa wakati katika shule walizopangiwa July 17 mwaka huu na kwamba hakutakuwa na mabadiliko ya shule walizopangiwa.

"Na kama kuna mwanafunzi ambaye hataripoti kwenye shule aliyopangiwa kwa muda wa siku 14 nafasi yake itachukuliwa na mtu mwingine," alisema Simbachawene.

Kuangalia majina ya wanafunzi na shule walizochaguliwa bofya hapa  www.tamisemi.go.tzauwww.moe.go.tz
Stori na EATV

Rayvanny wa WCB ameachia Video nyingine, inaitwa "Mbeleko".

$
0
0
Msanii kutoka lebo ya WCB, Rayvanny ameachia video mpya ya wimbo unaitwa ‘Mbeleko’, video imeongozwa na Joowzey, tazama hapa chini alafu toa komenti yako.

Amitabh Bachchan na mkewe 'Jaya' wakati wa ujana wao.

$
0
0
Staa wa filamu na muziki wa kihindi Amitabh Bachchan ambaye juzi kati amesherehekea miaka 44 ya ndoa yake na mkewe Jaya, kupitia ukurasa wake wa Twitter ametupia picha yake ya kitambo ya miaka 1973 ikiwa ni wakati akiigiza kwenye filamu ‘Zanjeer’.

Amitabh ameandika katika picha hiyo>>>, “a shoot from 'Zanjeer' and the wifely instincts leap up .. the way to a man's heart is via his stomach .. we were not married then”.

Jaya Bachchan anaonekana akimlisha mchumba wake Amitabh kwa mikono yake, Japo wakati huo walikua bado hawajaoana.

Fahamu gari lenye kasi zaidi duniani kwa mwaka 2017.

$
0
0
Gari lenye mwendo wa kasi zaidi duniani litakimbia kwa mara ya kwanza kabisa tarehe 26 mwezi Oktoba. 

Gari hilo litakimbia kwa kasi ya chini wakati wa majiribio kwenye uwanja wa ndege wa Newquay huko Conawall.
 
Wahandisi wanataka kukagua mitambo yote ya gari hilo kabla ya kulipeleka nchini Afrika Kusini mwaka ujao, kukimbia kuvunja rekodi ya mbio ya kasi zaidi ardhini.

Kwa sasa rekodi ya kasi ardhini ni 763mph au 1,228km/h, na gai hilo linalofahamika kama Bloodhound litaongeza kasi kwanza hadi 800mph na kisha 1000mph.

Majaribio ya Newquay hayatafikia kasi kama hiyo kwa kuwa barabara ya mita 2,744 ni fupi kiliwezesha Bloodhound kushika kasi.

Badala yake dereva Andy Greren, ataliendesha gari hilo kwa kasi ya 200mph likitumia injini ya ndege aina ya Eurofighter-Typhoon

Itakua siku ngumu kwa Dereva Andy Green kwa sababu itakuwa mara yake ya kwanza kuliendesha gari hilo.

Matarajio ni kuwa Bloodhoundlitapelekwa eneo la Hakskeen Pan huko Northen Cape nchini Afrika Kusini kwa muda wa mwaka mmoja hivi unaokuja kajaribu kutimiza lengo lake.

Ili hilo liweze kufanyika, awamu nyingine ya uundaji wa roketi hiyo ni lazima ukamilike.
Na bbc

Waigizaji 10 wa kike kutoka India wanaoongoza kwa mwaka 2017.

$
0
0
1. Deepika Padukone alizaliwa 5th January, 1986. Ni muigizaji wa filamu za kihindi na model mwenye mafanikio katika mastaa wa Bollywood.

Movie zake tano alizocheza na zinazosumbua kwa sasa ni pamoja na Bajirao Mastani, Tamasha, Piku, Happy New Year,and Finding Fanny.
2. ANUSHKA SHARMA
Anushka Sharma was born on the 1st of May, 1988. She is an Indian film actress and producer who has established a career in Hindi cinema. She is also one of the most popular actresses in India as well. Her previous 5 films including Sultan, Dil Dhadakne Do, Bombay Velvet, NH10, and Pk. nominations as wel
3. ALIA BHAT
Alia Bhatt was born on 15th of March, 1993.
She is an Indian actress who appears in Bollywood films. 

Her previous 5 films including Udta Punjab, Kapoor and Sons, Shaandaar, Humpty Sharma Ki Dulhania, and 2 States. She won the Filmfare Critics Award for Best Actress and also received a Best Actress nomination at the same ceremony as well. 

Being the one of the best Bollywood actresses, Bhatt is a very successful woman.
4.SHRADDHA KAPOOR
Shraddha Kapoor was born on 3rd of March, 1989. She is an Indian film actress and singer who works for Bollywood films. Kapoor is one of the finest young talent of Bollywood who is doing well in film industry from past two years. Her previous 5 years including Baaghi, ABCD 2, Haider, Ek Villain, and Aashiqui 2.
5. KATRINA KAIF
Katrina Kaif Was born on 16th of July, 1983. She is a British-Indian film actress and model. 
Primarily known for her work in Bollywood films, Kaif has also appeared in Telugu and Malayalam films as well. 
At the age of fourteen, Katrina won a beauty contest in Hawaii, and received her first modelling assignment in a jewelry campaign.
 Her pervious 5 films including Fitoor, Phantom, Bang Bang, Dhoom 3, and Jab Tak Hai Jaan.
 
6. PRIYANKA CHOPRA
Priyanka Choprawas born on 18th of July, 1982. She is an Indian film actress and singer as well as the winner of the Miss World Pageat in 2000. Her previous 5films including Jai Gangaajal, Bajirao Mastani, Dil Dhadakne Do, Marry Kom, and Gunday. Also, she is noted for her philanthropic work, and appointed as a UNICEF Goodwill Ambassador for Child Rights in 2010. 

7. KANGANA RANAUT - Alizaliwa 23, Machi 1997
8. KAREENA KAPOOR KHAN - Alizaliwa 21 Septamba 1980
9. VIDYA BALAN - Alizaliwa - 1 Januari 1978
10. SONAM KAPOOR - Alizaliwa - 9 June 1985

Top 10 ya mastaa wakike wenye macho mazuri zaidi duniani.

$
0
0
Macho ni kiungo ghari na muhimu katika uso wa mwanadamu. Sasa leo wakwetu nimekutana na hii ya mastaa wakike duniani wenye macho mazuri zaidi, huenda wewe ukawa unawako unaye mfahamu, lakini hawa ni wale 10 maarufu waliotajwa.

Wanasema macho ya mwanamke ni asset nzuri zaidi katika mwili wake. Kwani anaweza kuonyesha hisia zake na furaha yake kupitia macho, anaweza kuongea kwa kwa kutumia macho na ukamuelewa. Ni ngumu sana kukutana na macho mazuri, lakini sasa cheki hawa wakali hapa>>> 

10. CHARLIZE THERON
Charlize Theron ni muigizaji na mwanamitindo kutoka Afrika ya Kusini. Alianzia kazi ya uigizaji Marekani na kuwa maarufu miaka ya 1990 hivi . Ana macho mazuri. Pia amekwisha kushinda tuzo ya Oscar kama Best Performance kama staa wa kike katika filamu ya Monster.

9. MILLA JOVOVICH
Milla Jovovich ni mwanamitindo, muigizaji, mwanamuziki na mbunifu wa mavazi. Katika kazi zake amekwishaonekana katika filamu za kiasayansi na zile za action huku katika muziki akipewa umaarufu kama “reigning queen of kick-butt”.

8.CELINA JAITLEY
Celina Jaitly ni muigizaji wa kike kutoka India ambaye amekua akionekana katita filamu za Bollywood. Pia Celina alikuwa ni beauty queen na model pia, amekwisha shinda mashindano ya umiss na kutwaa taji la Femina Miss India Universe mwaka2001.

 7. KRISTIN KREUK
Kristin Laura Kreuk ni muigizaji na muandaaji mkuu wa filamu kutoka Canadia. Ukitaka kumfahamu vizuri zaidi, cheki series ya kimarekani inayoitwa Smallville, ameigiza kama Lana Lang

6. GIADA DE LAURENTIIS
Giada Pamela De Laurentiis ni mpishi, mwandishi, na mtangazaji wa Tv Imuitalia na mmarekani. Anakipindi chake cha kinachohusu mapishi ambacho huruka kila siku katika Food Network tangu 2003.

5. AUDREY HEPBURN
Audrey Hepburn alikuwa ni muigizaji na liyejihusisha na masuala ya kijamii kutoka Uingereza. Audrey alishawahi kushinda tuzo ya  Oscar kama muigizaji bora wa kike.

4. ELIZABETH TYLOR
Dame Elizabeth Rosemond “Liz” Taylor, DBE alikuwa ni muigizaji wa kike mwenye asili ya British-American. Ameshawahi kushinda tuzo mbili za Oscars, moja wapo ikiwa ni kuhusu macho yake mazuri. 

3.KRISTIN STEWART
Kristen Jaymes Stewart ni muigizaji wa kike kutoka Marekani, maarufu kama staa aliyecheza Bella Swan katika movie ya The Twilight Saga. Kristen Stewart ana macho yenye mvuto ambayo kila mtu atanasa akimtazama.

2. ANGELINA JOLIE
Angelina Jolie ni muigizaji na muongozaji wa filamu kutoka Marekani. Angelina amekwisha shinda tuzo ya Academy, mbili za Screen Actors Guild Awards, na tatu za Golden Globe Awards, yeah macho yake yanamvuto na midomo yake yakuvutia. Angelina ni binti ya Jon Voight na amekwisha wahi kushinda tuzo ya Oscar kama muigizaji msaidizi bora wa kike.

1. AISHWARYA RAI
Aishwarya Rai ni muigizaji maarufu wa filamu kutoka India. Mwanzoni alifanya kazi kama mlimbwende/model, na hatimae akashinda Miss World pageantmwaka 1994

Hakika macho yake yanadhirika kuwa yenye mvuto dunia nzima na kumfanya kushika nafasi ya kwanza katika mastaa wa kike wenye macho mazuri zaidi duniani.

Aishwarya alikwisha kuchaguliwa na Time magazine mwaka 2004 kama mmoja kati wa "watu 100 wenye ushawishi duniani" na anatambulika pia kama mwanamke mrembo zaidi duniani.

Je unamaoni gani kuhusu hii orodha iliyoandaliwa na mtandao wa wonders list?

Vitabu 17 kilamtu duniani anavyopaswa kuvisoma kwa mujibu wa tajiri namba moja duniani Bill Gates.

$
0
0
1. Tap Dancing to Work: Warren Buffett on Practically Everything, 1966-2012 by Carol Loomis

Kwamujibu wa Jarida la Forbes, Warren Buffett ndiye tajiri namba mbili duniani kwa mwaka 2017 akiwa na utajiri wa dola za kimarekani bilioni 75.6, hukuBill Gatesakiongoza kwa utajiri wa dola za kimarekani bilioni 86.
Huyo ndiye Bill Gates anayekupa maono ya kupitia hivi vita 17 ambavyo vingi vina nguvu ya mafanikio katika maisha.

2. Making the Modern World: Materials and Dematerialization by Vaclav Smil
3. The Sixth Extinction: An Unnatural History byElizabeth Kolbert
4. Stress Test: Reflections on Financial Crises by Tim Geithner
5. The Better Angels of Our Nature: Why Violence Has Declined by Steven Pinker 
6.The Man Who Fed the Worldby Leon Hesser
7. Business Adventures: Twelve Classic Tales from the World of Wall Streetby John Brooks
8.The Bully Pulpit:Theodore Roosevelt, William Howard Taft, and the Golden Age of Journalismby Doris Kearns Goodwin
9.The Rosie Project: A Novel by Graeme Simsion
10.On Immunityby Eula Biss
11. How Asia Worksby Joe Studwell
12. How to Lie with Statistics by Darrell Huff
13. Epic Measures by Jeremy Smith
14. Stuff Matters by Mark Miodownik
15.Hyperbole and a Half by Allie Brosh
16. What If? by Randall Munroe
17. Should We Eat Meat?by Vaclav Smil

Hivi ndivyo vitabu 17 ambavyo tajiri namba moja wa dunia, anakushauri uvisome. Karibu Asili Yetu Tanzania.

Beyonce na Jayz wapata watoto mapacha.

$
0
0
Mastaa wa muziki duniani kutoka Marekani yani Beyonce Knowles na Sean Carter 'Jay Z'inavyosemekana wamewakaribisha mapacha wawili, baada ya Bey kutumia muda wake wa ujauzito kikamilifu na kuweza kujifungua salama, huku watoto wakiwa na afya njema kwa mujibu wa mtandao wa 'TME'.

Kwa vyanzo mbali mbali vya kimataifa, vimeeleza kuwa waili hao bado hawajasema chochote, kuhusu Bey kujifungua, ila inasemekana mambo tayari, na muda ukifika watatuwekea watoto hadharani tuone wamechukua sura kwa nani, baba au mama. 

Blue Ivy Carter ni mtoto (binti) yao wa kwanza, toka wanandoa hao wenye nguvu zaidi duniani kufunga ndoa mnamo mwaka 2008, na kumkaribisha binti yao wa kwanza aitwae Blue mwezi  January 7, 2012.

Baba yake Beyonce, Mathew athibitisha kuzaliwa kwa watoto mapacha wa mastaa Jayz na Beyonce.

$
0
0
Baada ya kusambaa kwa tetesi za Beyonce na Jay Z kupata mapacha.
 Baba mzazi wa Queen Bey ambaye pia aliwahi kuwa meneja wake, Mathew Knowles amethibitisha hilo.

 Jumapili hii  Knowles aliweka picha ya kadi kwenye mtandao wa Twitter akipongeza kuzaliwa kwa mapacha hao na kuandika, “They’re here! #beyonce #twins #jayz #happybirthday.”

Katika kuthibitisha jambo hilo ni kweli, baba huyo wa msanii Beyonce aliweka picha hiyo hiyo kwenye mtandao wa Instagram na mama yake Beyonce aliweza ku-like picha hiyo.

Kwa mujibu wa TMZ, inadai kuwa watoto hao wamezaliwa Jumatatu iliyopita ya Juni 12 lakini mpaka sasa bado wapo hospitalini hawajaruhusiwa wakiwa chini ya uangalizi pamoja na mama yao.
Blue Ivy Carter ni mtoto (binti) yao wa kwanza, toka wanandoa hao wenye nguvu zaidi duniani kufunga ndoa mnamo mwaka 2008, na kumkaribisha binti yao wa kwanza aitwae Blue mwezi  January 7, 2012.

Mji wenye maisha ya juu zaidi duniani, unapatikana Afrika.

$
0
0
Tumezoea kuona na kusikia tafiti nyingi zikifanyika huku zikiiacha Afrika mikono mitupu, labda tu kwa zile tafiti za upande wa kushoto ndiko tunakowekwa.

Sasa nikujuze kuwa utafiti uliofanywa na Shirika la Takwimu za Gharama za Kuishi Duniani (Mercer) umeutaja mji mkuu wa Angola, Luanda kushika nafasi ya kwanza duniani kati ya miji yenye gharama kubwa zaidi za kuishi.
Takwimu hizi zimetolewa na shirika la Mercer ambalo lilifanya utafiti. Katika takwimu hizo miji ya Tokyo, Zurich na Singapore pia nayo inachukua nafasi tano za kwanza. 

Mji wa London ulishuka hadi nafasi ya 30 hasa kutokana na kushuka kwa thamani ya paundi.

Utafiti huo wa kila mwaka huangazia masuala kadha kando na gharama ya kukodi nyumba. Utafiti huo huangazia gharama ya vitu 200 kwa kila mji, ikiwemo nyumba, usafiri, mavazi, chakula na burudani.
Tazama nchi nyinginezo hapo chini>>>
 

Kanye West kumlipa kitita cha dola mwanamke mwingine ili amzalie mtoto badala ya mkewe Kim Kardashian.

$
0
0
Kila siku vituko na matukio yanazidi kuwa makubwa hasa kwa watu maarufu duniani.

Unaambiwa familia ya Kanye West imempata mtu ataweza kubeba ujauzito wa Kim Kardashian ili waweze kupata mtoto wa tatu.
Kim na Kanye wamekubaliana kumlipa malipo ya dola 45,000 kwa miezi kumi ni sawa na dola 4,500 kwa kila mwezi.

Mtu huyo pia amepewa mashariti ya kutokunywa kilevi, kuvuta sigara na kutumia dawa yoyote yatakayo weza kuaharibu mimba hiyo.

Kampuni ambayo inashughulika na project hiyo itahakikisha mbeba mimba huyo nakula vizuri na kepuka madhara yoyote yataka pelekea mimba kutoka. 

Hata hivyo bado haijatajwa ni kampuni gani itahusika na wala ni nani atabeba mimba hiyo.

Huwenda mastaa hawa wakawa wamehamasika kuongeza familia, ikiwa ni baada ya siku chache mastaa Jayz na Beyonce kuweza kupata mapacha.

Video: I Miss You - Diamond Platnumz

$
0
0
Mwimbaji wa Bongofleva kutoka WCBDiamond Platnumz ametusogezea burudani mpya kupitia wimbo wake wa ‘I miss You‘ ikiwa ni miongoni mwa video mpya za mwezi June, 2017 zitakazo ipa kampani siku yako imalizike uzuri.

Unaweza kuitizama hapa chini>>>

Video: Diamond Platnumz Ft. Tiwa Savage - "Fire".

$
0
0
Mwimbaji staa wa Bongo Diamond Platnumz amefanya collabo na mwimbaji staa kutoka Nigeria Tiwa Savage ni katika video ya wimbo unaoitwa 'Fire'>>>

Hii hapa ndio video yenyewe ya mkali huyu ambaye ni mmiliki pia wa Lable ya WCB - Diamond Platnumz  umeipokea vipi hii wakwetu>>>

Movie mpya ya Jackie Chan 2017, James Bond atinga ndani.

$
0
0
Baada ya mtaalamu na mkongwe wa movie za Kung Fun maarufu kama Jackie Chan kufanya poa na movie yake ya 'Kung Fu Yoga'aliyoigiza na wakali kutoka India, sasa nakusogezea hii stori kuhusu ujio mwingine wa movie yake mpya.
Jackie Chain ambaye atakutana tena uso kwa uso na Pierce Brosnan, ambaye amewahi kuigiza kama James Bond, utawaona katika muvi mpya inayoitwa ‘The Foreigner’ itakayo zinduliwa rasmi ifikapo Septemba 30 mwaka huu.
Jackie Chain na Pierce Brosnan, wamewahi kuigiza pamoja katika muvi kama vile'Die Another Day', 'The World Is Not Enough'  na nyinginezo.

Nay Wa Mitego aja tena na wimbo huu "Moto". mp3

$
0
0
Msanii wa muziki wa hip hop, Nay wa Mitego ameachia wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la ‘Moto’ huku producer akiwa ni Awasome.

Nini mtizamo wako baada ya kusikiliza wimbo huu kutoka kwa Nay? Tuachie maoni yako hapo wakwetu>>>

Usikilize hapo chini>>>>
Viewing all 3608 articles
Browse latest View live




Latest Images