Quantcast
Channel: Www.maxwellyblogspot.com
Viewing all 3608 articles
Browse latest View live

DARASA FT. O'SMAN - "HAKI SAWA" (WIMBO MPYA).

$
0
0
SIKILIZA WIMBO HUU HAPA.......
.

WAPIGIE KURA "JAMBO SQUAD" KUWA KUNDI BORA LA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA.

$
0
0
Kama wewe ni mshabiki wa ukweli wa kundi zima la Jambo Squad kutoka A Town, ukiwa unaguswa na ngoma zao kibao kama "Mamong'oo, Tukunyema na nyinginezo nyingi, fuata maelekezo hapo juu.

J4C FT. ESLYNE - "NISIKILIZE MIMI" (NI WIMBO MPYA).

$
0
0
UNAWEZA KUUSIKILIZA WIMBO HUU HAPA.......

PICHA ZA "DIAMOND PLATNUMZ" NDANI YA "SPORAH SHOW".

$
0
0
Platnumz akiwa ndani ya show ya Sporah.






Diamond Platnumz  kwaujumla ni "WASAFI CREW"

WASAFI CREW NDANI YA SPORAH SHOW

BOB JUNIOR - "KIMBIJI" NI WIMBO WAKE MPYA, USIKILIZE HAPA.

$
0
0
SIKILIZA WIMBO MPYA WA BOB JUNIOR - SHAROBARO PRESIDENT.

LADY JAY DEE ATOA WOSIA WAKE KABLA YA KIFO.

$
0
0
"JIDE"
Watu wanashtuka mtu akiongelea kifo, Utafikiri hawafahamu fika kuwa kila nafsi itakionja, Kwenye maisha yangu nimepitia mambo mengi, magumu na mepesi Na bado naendelea ku experience mambo magumu zaidi kadri ninavyozidi kuwa mkubwa.

Siku za karibuni nimekuwa nikipigwa vita sana na watu wenye uwezo mkubwa kifedha , ki umri na hata wenye ukubwa wa connection katika hii industry ya muziki. Wanaomiliki chombo cha habari.
Nasimama na kusema kuwa sitokata tamaa, kwani lengo lao kubwa ni kuona na kuhakikisha nimeanguka kabisa na sipo katika ramani ya muziki.
Watu hao ambao vita yao ilikuwa baridi miaka kumi iliopita, sasa inazidi kuwa moto baada ya kutambua kuwa mimi ni mtu mwenye maamuzi yangu na misimamo yangu bila kuburuzwa.

Wanapita kila mahali kuhakikisha kila mrija unaoniingizia chochote unakatika, na hiyo ni kutaka kuuthibitishia umma wa Tanzania kuwa hakuna msanii anaeweza ku survive bila wao.
Mimi ni msanii tofauti na hao mnaofikiria.Nadhani mnafahamu tangu niachane na Tuzo zenu mnazo influence nani apate nani asipate, na tangu niachane na Fiesta nilipolipwa laki 8 mara ya mwisho na kuamua kuunda Band ili nijiajiri na kupata shows zangu mwenyewe, ikafanikiwa sana jambo ambalo limewauma na kuamua kufanya kitu cha kuiangusha Band yangu.
Nita survive kwa njia zozote MUNGU alizonipangia.Wakati bado wote tunapumua na kwakuwa watu hao hawanipendi kabisa, Naamini fika hawataweza kunipenda hata siku nitakapokuwa nimekufa.
Na huu ndio wosia wangu kwa watu hao.
Natambua wanaweza kutumia redio yao kutangaza sana kifo changu na kusema marehemu alikuwa mtu mzuri na pengine kupiga nyimbo zangu kuanzia asubuhi mpaka jioni.
Ila naomba nitamke hivi, siku nikifa CLOUDS FM isipige nyimbo zangu, wala isiongelee lolote kuhusiana na kifo changu.
Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga wasihudhurie msiba wangu, na mkiwaona muwapige wame. Enyi mtakaokuwa hai baada yangu.
Kama wamenifitini, na hawajanipenda nikiwa hai. Hakuna haja ya kujifanya kunipenda nikiwa marehemu.
Sina haja wanipende pia kwakuwa mimi sio ndugu yao, Ila ubaya wanaoundeleza mioyoni mwao wanaujua na nina hakika nafsi zao zinawasuta pia.
Niliamua kujiepusha nao miaka mingi na kufanya biashara zangu, nimekaa kimya watu wanafikiri nabebwa lakini sijabebwa chochote sikutaka ugomvi haya mambo yalianza baada ya Album yangu ya pili ya Binti mwaka 2003 nilipojitoa Smooth Vibes chini ya Ruge.
Nilivumilia fitna nikiamini ipo siku yatakwisha lakini naona moto ndio unazidi kuwaka.
Na hii ni kwasababu wanaogopa msanii akiwa mkubwa watashindwa kumuamrisha, Hamuwezi kumiliki dunia..
Kama mnasema mlinibeba mbona hamkuwabeba dada zenu wa tumbo moja waimbe ili hela irudi nyumbani??. kama kweli wewe Kusaga unajua kubeba basi beba jiwe liimbe liwe star..
Kwa roho zenu mbaya mnaweza kumbeba mpita njia nyie??.Talent haibebwi, hujibeba kama mnabisha si mna watoto wabebeni basi wawe kama kina Diamond ndio nitaamini kweli nyie mnaweza kubeba watu.
Mnawatishia wasanii kuwa yoyote atakaefanya nyimbo na mimi hazitapigwa, vikao vinne mmeshakaa kunijadili.
Mnadhani je! nitapungukiwa nini endapo wasanii wengine wakiacha kufanya kazi na mimi?? nyimbo hazitakuwa nzuri.
Basi sawa ngoja tuone MUNGU ni nani, Binadamu nani?? Kwahiyo mtaamrisha watu pia wasikae na mimi??
Ilikuwa niseme majina matatu huyo mmoja nimemsamehe baada ya kugundua sio hiyari yake ila yuko under influence ya hawa jamaa wawili.
Kila siku mnamsingizia Ruge peke yake Kusaga ni mfitini kuliko hata huyo Ruge, watu hamjui tu.
Mtu hela zote hizo bado shillingi mbili ya Jide inakuuma?? Roho gani hiyo??
Naishia hapo na sitabatilisha kauli yangu.
JIDE

JOSLIN - "ITIKA" - HUU NI WIMBO WAKE MPYA, USIKILIZE HAPA.

$
0
0
Unaweza kuusikiliza wimbo mpya wa Msanii Joslin unaofahamika kama "Itika" ukiwa umetengenezwa na Producer "Tiddy".

LADY JAY DEE ATOA ORODHA YA MAJINA YA WASANII WATAKAO SHIRIKI SHOO YAKE.

$
0
0
List ya wasanii ambao watamshindikiza Lady Jaydee aka Komando aka Anaconda kwenye sherehe za miaka 13 na uzinduzi wa Album yake mpya ya 6 'Nothing but the Truth'.

Kwa mujibu wa ukurasa wa facebook wa Lady Jaydee wasanii ambao wataperform ni TID, Hamza Kalala, Barnaba, Grace Matata,Linah,Profesa Jay na MatonyaItakuwa ni tarehe 31 May kama unavyoona kwenye Posters pande za Nyumbani Lounge.Tickets za show ya miaka 13 ya LADY JAYDEE za VIP, 50,000/= zitaanza kuuzwa tarehe 10 May 2013. 

Katika ticket hii utapata Dinner, Wine zitakuwepo mezani pamoja na free CD Album mpya.
Meza ziko 50 tu zenye viti 10@. Wahi nafasi yako mapema.

Ticket zingine za 20,000/= zitauzwa mlangoni siku ya show ambayo ni tarehe 31 May 2013
Na utapata CD Album ya Nothing But The Truth Bureeeee.


Chanzo unaweza kutembelea..... AnnaPeter.com

VIDEO: ROSE NDAUKA AKIZUNGUMZIA MOVIE YAKE MPYA YA "BETTER TRUTH" ITAKAYO TOKA SOO.

$
0
0
Best Actress wa bongo movie “Rose Ndauka” akiongelea kuhusu movie ya better truth inayotarajiwa kutoka siku za hivi karibuni.
Wale wote wapenzi wa bongo movie sasa kaeni tayari kwa kitu hichi kipya cha Rose Ndauka.

Chanzo: BaabKubwa Magazine

ITV HABARI: SERIKALI YAFUTA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE YA MWAKA 2012.

$
0
0
Serikali imefuta matokeo ya mtihani wa kidato na nne cha mwaka 2012 na kuamuru yaandaliwe upya kwa kufuata utaratibu uliotumika mwaka 2011.

Chanzo: ITV TANZANIA

EPISODE YA 54 - "TAMTHILIA YA MARA CLARA" – GARY ADHAMINIWA HUKU AMANTE NAE ATOKA HOSPITALI, WOTE WAKUTANA.

$
0
0
MARA

Amante apata fahamu na kuongea na Alvira, wote waombana msamaha na kurudiana, lakini kwa upande wa Gary hali bado ni tete, kwani anampigia simu Clara ili amdhamini kutoka polisi.

Clara afanikiwa kumtoa baba yake polisi, lakini anajaribu kumshinikiza wahamie nyumba nyingine kwani hiyo ni mbaya, lakini Gary hajakubaliana na wazo hilo kabisaaa!.

Gary anampigia simu Alvira na kumtaka wakutane kwa maongezi lakini, Alvira anakataa na kusema yeye ndio chanzo cha mambo yote yaliyotokea, akaongeza  kwa kusema “nenda kuzimu”.

Clara aenda hospitali kuomba wazuie kesi ya baba yake Gary isipelekwe mahakamani, lakini maombi hayo yanatupiliwa mbali na familia ya Amante, aondoka hospitali kwa hasira.

 MARA na SUZAN wanaenda kumuona mama yake Gary mwenye ugonjwa wa kupooza, wanamuuliza kama Clara anajua au anashiriki katika maovu ya Gary? Pia bibi huyo anaomba waondoke naye, wanafanikiwa kutoroka nae na kutokomea kusikojulikana.

Gary anarudi na kumuuliza mlezi wa mama yake (Mrs. David) kwa ukali huku akimkaba shingoni, “mama yangu yukowapi?”  Anaamua kumfukuza ili akamtafute mama yake hadi ampate kwani asipompata atamuua. Gary na Clara wanaamua kwenda kuripot polisi, lakini polisi wanamwambia hawawezi kumtafuta mtu yeyote anayedhaniwa kupotea hadi masaa 24 yapite. Gary anakasilika na kuanza kujibizana na polisi, lakini Clara anamwepusha na kuondoka kituoni hapo.

MARA na Suzan wafanikiwa kumtorosha mama yake Gary na kwenda nae katika nyumba mpya ya Alvira, huko nyumbani bibi huyo anaanza kupata nafuu ya kuweza kuongea. Amante anatoka hospitali na kujumuika na familia yake upya, lakini Amante anaanza kumuuliza mama yake Gary kuhusu maovu ya mwanae ili apate ushahidi wa kumtupa jela.

Gary, Clara wote wanakutana na familia ya Amante uso kwa uso, sasa nini kitatokea kati yao?

Je nini kitaendelea? Tazama Star TV na karibu tena kwa dondoo  nyingine za tamthilia hii hapa hapa.

HAWA NDIO AKINADADA WA KUNDI LA "TLC" LINALOUNGANA TENA.

AY Feat. FID Q - "JIPE SHAVU", USIKILIZE WIMBO HUU MPYA.

$
0
0
Huu ni wimbo mpya wa AY akimshirikisha FID Q, ngoma inaitwa "Jipe Shavu", Usikilize hapo chini.

MSANII SIZE 8 AANZA KUWEKA WAZI ULOKOLE WAKE KENYA.

$
0
0
Msanii wa kike ambaye hivi karibuni amejitangaza kuokoka na kuanza kufanya kazi ya kulieneza neno la Mungu Size 8 hivi sasa amejiandaa kutumbuiza katika tamasha lake la kwanza tokea ajitangaze kuokoka kwake.
Size 8 atawapagawisha mashabiki na kibao chake kipya kiitwacho mateke ambacho kimekuwa hit kwa mwaka huu wa 2013 hadi hatua ya kushika nafasi ya kwanza katika chati kali za nyimbo za gospel.


Itakumbukwa kuwa Size 8 alitamka kuwa ataachana na vijivazi hivyo ila ukweli wote ni hapo jioni katika tamasha hilo kubwa na la aina yake.


Story na BaabKubwa Magazine

INASEMEKANA LIL WAYNE AMEMVISHA PETE YA UCHUMBA MPENZI WAKE WA KIITALIANO.

$
0
0
Kwa habari ambazo zinazidi kuenea mitandaoni zinasema kuwa, pamoja na staa huyu wa miondoko ya rap maarufu kama Lil Wayne, amemvisha pete ya uchumba demu wa kiitaliano.

Kama ilivyobainishwa na mtandao mmoja wa ughaibuni unaokwenda kwa jina la XXL, umesema kuwa Wayne pamoja na matatizo yake ya kiafya yaliyomtokea hivi juzi, jamaa huenda hivi karibuni akawa mume wa mpenzi wake wa tokea mwaka 2011 anayeitwa Dhea.

MILA KUNIS ATAJWA NA JARIDA LA "FHM" KUWA NDIYE MWANAMKE MREMBO WA KWANZA KWA MWAKA WA 2013 AKIFUATIA NO.2 RIHANNA.

$
0
0
 Baada ya Mila Kunis kutajwa na jarida la Esquire mwaka 2012 kama "Mwanamke mrembo anaye Ishi", Mila Kunis pia ametunukiwa heshima na Jarida moja la Uingereza la FHM, kama "Mwanamke mrembo duniani" kwa mwaka wa 2013, huku namba mbili ikienda kwa Rihanna.

             Mila Kunis akiwa katika pozi linalomuonyesha muonekano wa maumbile yake halisi.

RIHANNA

BOMU LALIPUKA KATIKA KANISA KATOLIKI LILILOKO OLASITI - ARUSHA.

$
0
0

Habari zilizoifikia blog ya Asili Yetu Tanzania zinasema kuwa "Kanisa katoliki jimbo la Arusha lililopo olasiti linaloitwa MT YOSEPH MFANYAKAZI limepigwa bomu,na kujeruhi waumini wengine wengi, ni katika ufunguzi wa kanisa hilo jipya ambalo lilikuwa linafunguliwa na Balozi wa papa nchini Tz papa Fransinco kadili, hivi sasa askari wamezunguka eneo hilo!"

Hadi sasa bado taarifa kamili kutoka Jeshi la polisi Arusha bado haijatolewa, endelea kufuuatilia kwa taarifa hiyo zaidi hapa hapa.

Na Mwandishi wetu THOMAS ADAM

MLIPUKO WA BOMU KATIKA KANISA KATOLIKI ARUSHA, MWAKILISHI WA PAPA ANUSULIKA.

$
0
0

Habari zilizopatikana hivi punde zinaeleza kuwa kumetokea mlipuko wa kitu kinachodhaniwa kuwa bomu katika Parokia mpya ya OLasiti  katika jimbo kuu la Arusha. Inaelezwa na baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo lililotokea saa tano kasoro asubuhi kuwa watu kadhaa wamejeruhiwa na wamekimbizwa hospitali kupata matibabu.

kamanda wa jeshi la polisi Mkoani Arusha Liberatus Sabas amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa mpaka sasa hakuna mtu aliyepoteza maisha kufuatia tukio hilo.


"Mlipuko umetokea vyombo vya usalama vipo hapa kufanya uchunguzi ,siwezi kukupa idadi ya majeruhi kwa sasa ,ninachoweza kukuambia hakuna mtu aliyepoteza maisha na Balozi wa Vatican yu salama"alisema Sabas kwa njia ya simu.


Habari kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa bomu hilo lilirushwa na watu waliofika karibu na kanisa hilo wakivalia nguo za kuficha nyuso wakiwa katika gari ambayo namba zake hazikuweza kufamika na kurusha kitu ambacho kililipuka karibu na meza ya misa takatifu.

Misa hiyo ilikuwa inaendeshwa na Balozi wa Papa nchini Tanzania .
Watu  kadhaa wamejeruhiwa ibaya  katika ibada hiyo.

Hakuna taarifa za kifo  iliyothibitishwa na mamamlaka za za usalama bado.
Maafisa wa jeshi la polisi ,askari wa jeshi la wananchi kikosi cha mabomu wapo katika eneo la tukio.


Tutaendelea kuwahabarisha kile kinachotokea
Habari na NGEREZA 

NIKKI MBISHI - "NEY WA MITEGO", HUU NI WIMBO MPYA.

$
0
0
SIKILIZA WIMBO HUU HAPA.......

JAGUAR - "KIPEPEO" (OFFICIAL VIDEO).

$
0
0
Hii ndio video mpya ya msanii kutoka Kenya Jaguar ya wimbo wake 'Kipepeo
Viewing all 3608 articles
Browse latest View live




Latest Images